Mahubiri ya Jumapili · Kipindi cha Kawaida, Mwaka C, Sehemu 13 · Luka 7:11–17
Mjane wa Naini
Padre Anthony Wekesa ·
Sauti na video
Hakuna rekodi iliyoambatishwa na mahubiri haya.

Bwana wetu anakutana na msafara wa mazishi kwenye lango la mji. Hakuna aliyemwita wala aliyemwomba kitu.
Anamwona yule mjane, na Injili inasema alimhurumia. Neno hilo linatangulia muujiza. Lolote tunaloombwa kufanya kwa wafiwa katika parokia hii huanzia hapo — kwa kutoka nje kuwalaki langoni.
Sambaza hiiWhatsAppBarua pepe