Onyesho — kila jina na kila takwimu hapa ni ya kubuni Demonstration — every name and figure here is fictional

Onyesho hili hurudi kwenye maudhui yake ya awali kila usiku, kwa hivyo chochote unachoweka hapa hakitakuwepo asubuhi. This demonstration returns to its seeded content every night, so anything you enter here is gone by morning.

Rukia yaliyomo
St. Monica's Catholic Church, Mwavuli

Maisha ya parokia

Harambee ya paa jipya

Parish Office ·

Picha

Halmashauri ya parokia ilikutana Jumapili baada ya Misa ya saa tano na nusu na kupanga harambee ya paa kufanyika Jumapili tarehe ishirini Septemba, kuanzia baada ya Misa ya pili hadi alasiri.

Paa juu ya madhabahu limekuwa likivuja tangu masika, na mabati juu ya sakristia hayafai tena kukarabatiwa. Bei tatu zilisomwa kwa halmashauri; kazi inatarajiwa kuchukua wiki nne itakapoanza.

Ahadi zinaweza kutolewa kwa mjumbe yeyote wa halmashauri, ofisini wakati wa kazi, au kwa M-Pesa kupitia paybill ya parokia. Kila ahadi hupewa risiti, na jumla itatangazwa Misani kila Jumapili hadi kazi ikamilike.

Sambaza hiiWhatsAppBarua pepe